Baada ya kocha Mwinyi Zahera kuwasili kutoka DR Congo alikokuwa akitimiza na majukumu ya timu ya Taifa, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea jijini Mwanza tayari kuwakabili Mbao Fc mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba Jumanne, Oktoba 22 2019
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema baada ya mchezo huo, wataendelea na maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Oktoba 27
Aidha Ten amesema tayari wamepokea taarifa kutoka CAF kuhusu waamuzi wa mchezo huo ambao watatokea nchini Ivory Coast, Kamisaa wa mchezo akitokea Djibout
Waamuzi hao watawasili nchini Oktoba 25, siku mbili kabla ya mchezo
ADVERTISE HERE