Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inakabiliwa na kibarua cha kuiondosha Sudan kwao katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani
Mchezo huo utapigwa saa mbili usiku kwa saa za Tanzania
Tanzania iliwasili Sudan tangu juzi ambapo jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa El Merriekh, Omdurman ambao mchezo huo utapigwa

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 nyumbani, vijana wa Etienne Ndaiyiragije wanahitaji kushinda mchezo huo kuanzia mabao mawili ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali za CHAN kwa mara ya pili
Ndayiragije amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wamedhamiria kupindua matokeo huko Sudan
ADVERTISE HERE