Uamuzi wa kuupeleka jijini Mwanza mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Pyramids Fc, umepokewa kwa furaha na mashabiki wa timu hiyo kanda ya ziwa ambao wamejipanga kuandika historia
Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuwasili jijini Mwanza Jumapili, mashabiki wameanza mapema mikakati ya kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuipa sapoti timu yao ili iweze kushinda mchezo huo utakaopigwa Jumapili ya Oktoba 27
Mashabiki kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga na Tabora tayari wameanza mipango ya maandalizi ya kuelekea jijini Mwanza
Pamoja na kuwa bado zoezi la uuzwaji tiketi halijaanza, mashabiki wameonyesha utayari wakisubiri kutangazwa kwa viingilio pamoja na uuzwaji wa tiketi
Uongozi wa Yanga umesema tiketi zitaanza kuuzwa mapema kuhakikisha mashabiki wote wanakuwa na tiketi siku tatu kabla ya mchezo
Hakuna tiketi zitakazouzwa siku ya mchezo
Shamrashamra kuanza mechi dhidi ya Mbao Fc
Viongozi wa Matawi ya Yanga jijini Mwanza wamesema shamrashamra za maandalizi ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc zitaanza Oktoba 22 Yanga itakapocheza na Mbao Fc mchezo wa ligi kuu