Molinga kupokewa kifalme Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Oct 2019
Molinga kupokewa kifalme Mwanza

Mshambuliaji wa Yanga David Molinga, ameandaliwa mapokezi ya aina yake wakati timu hiyo itakapowasili jijini Mwanza kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao utakaochezwa Jumanne wiki ijayo.

Viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijini Mwanza, wamesema watahakikisha Molinga wanamwandalia mazingira ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

Wamesema wanataka kuona Molinga akifunga mabao matatu β€˜hat-trick’ dhidi ya Mbao katika mchezo huo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mhando Madega ambaye ni Katibu wa matawi ya Yanga, mkoani Mwanza, a,esema wapo katika maandalizi ya mwisho ya kuipokea timu yao.

Madega alisema timu yao inakabiliwa na michezo miwili, ikiwamo wa kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri utakaochezwa Oktoba 27, mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba.

Alisema kuekekea michezo hiyo, mashabiki wa jiji hilo wanahitaji kuona Molinga akiifunga Mbao FC kama alivyofanya kwa timu ya Pamba katika mchezo wa kirafiki uliochezwa hivi karibuni.

Alisema baada ya kushuhudia mabao yaliyokuwa yanafungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo katika Kanda ya Kanda ya Ziwa, safari hii ni zamau ya Molinga kufanya hivyo.

"Makambo alianza kuifungia Yanga alipokuja Kanda ya Ziwa na Molinga pia ameanza kufunga alipokuja Mwanza, sasa safari hii anarudi Mwanza atafunga hat-trick," alisema.

Katibu huyo alisema kwa sasa wanataka kuona Molinga akifunga mabao kuanzia matatu katika mchezo mmoja.

"Safari hii timu tunaiandaa vyema kuhakikisha inapata ushindi mkubwa ili kuuthibitishia ulimwengu namna gani watu wa Mwanza tunafanya kazi.

"Yanga itashinda kuanzia mabao mawili na kuendelea na tutaanzia kwa Mbao FC kutesti mitambo, wakijitahidi sana watafungwa mabao 3-0," alitamba.

Alisema mchezo wao dhidi ya Pyramids utakuwa mwepesi kwani kwa mikakati waliyoipanga, hawaoni kama wapinzani wao hao wa Misri wanaweza kuepuka kipigo.

"Tunawasihi wana Yanga waachane na propaganda za kuogopesha kuhusu Pyramids, tuwe kitu kimoja kuipokea timu yetu," alisema Madega.

Kwa hisani ya Bingwa, Imeandikwa na DAMIAN MASYENENE, MWANZA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’