Katibu wa Baraza la Wazee Yanga Ibrahim Akilimali amesema baadhi ya wachezaji wa timu hiyo 'wamefungwa', wanahitaji 'kufunguliwa' ili waweze kufanya vizuri
Mzee Akilimali ambaye kwa siku za karibuni amekuwa hasikiki sana kutokana na maradhi, amesema uongozi wa Yanga unapaswa kushirikiana na Wazee kwani wako tayari kutoa mchango wao katika jambo hilo
"Timu yetu haifanyi vizuri kwa sababu baadhi ya wachezaji wetu wamefungwa," amesema
"Usajili uliofanyika haukuwa mbaya, kuna wachezaji tumewanunua huko kwao wanawania tuzo lakini hapa wanaonekana si lolote"
"Bahati mbaya viongozi hawatupi ushirikiano. Sisi tunataka tufanye mambo yetu ili tuweze kufuzu makundi lakini wao hawana mpango wowote wa kutupa zaidi ya kutukimbia"
"Pamoja na kuuhamishia mchezo dhidi ya Pyramids Mwanza, sioni kama tutafanikiwa kwani tatizo bado lipo"
Miongoni mwa nyota waliotua Yanga wakiwa 'wamoto' ni pamoja na mshambuliaji Juma Balinya ambaye aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda msimu uliopita
Balinya aliteuliwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Uganda
Hata hivyo amekuwa na wakati mgumu tangu atue Yanga