Mashabiki kurudishiwa viingilio baada ya mchezo kuahirishwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Oct 2019
Mashabiki kurudishiwa viingilio baada ya mchezo kuahirishwa

Uongozi wa klabu ya Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya Selcom watarudisha viingilio kwa mashabiki waliokata tiketi kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Pan African uliokuwa upigwe leo kwenye uwanja wa Uhuru

Mchezo huo haukufanyika baada ya uwanja wa Uhuru kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tukio hilo lilikuwa nje ya uwezo wao, amewashukuru mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo

"Tunawashukuru mashabiki wengi waliokuja uwanjani, tulitamani mchezo uchezwe lakini isingewezekana kutokana na hali halisi ya uwanja"

"Tutazungumza na wenzetu (Selcom) kuona utaratibu mzuri wa kuwarudishia viingilio nashabiki wenye tiketi"

"Mchezo hauwezi kufanyika kipindi hiki kwani wenzetu Pan African wanaelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi daraja la kwanza wakati sisi tunajiandaa kuelekea jijini Mwanza," amesema Bumbuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’