Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema taarifa zinazodai klabu ya Pyramids Fc imepeleka malalamiko shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) ikipinga mabadiliko ya uwanja yaliyofanywa na Yanga, hazina ukweli wowote
Mwakalebela amesema hakuna malalamiko yoyote yaliyopelekwa na klabu hiyo CAF na hivyo mchezo utapigwa Mwanza kama ulivyopangwa
Mwakalebela amefafanua kuwa kabla ya kuanza mashindano kila timu ilitakiwa kuwasilisha viwanja viwili ambavyo watavitumia
Hivyo uwanja wa CCM Kirumba na Uwanja wa Taifa ndio viwanja rasmi ambavyo Yanga ilivichagua kuvitumia kwenye mashindano ya mwaka huu na vimethibitishwa
"Uwanja umeshathibitishwa, hatuna haja ya kuchanganya maneno, hakuna kinachobadilika mchezo utachezwa CCM Kirumba," amesema
ADVERTISE HERE