Walinda lango Metacha Mnata na Farouk Shikalo wameendelea kuaminiwa na mataifa yao baada ya kuziongoza timu zao za Taifa kwenye michezo ya kirafiki
Jana Shikalo aliiwakilisha Kenya akikaa langoni kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Msumbiji mchezo ambao Kenya ilikubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani

Leo Metacha amepata nafasi ya kuanza akimuweka nje Juma Kaseja kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rwanda
Metacha alin'gara kwenye mchezo huo akiokoa mipira mingi ya hatari na kuisaidia Stars kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Makipa hao watakuwa na 'battle' ya aina yake kwenye kikosi cha Yanga
ADVERTISE HERE