Ushindi wa mabao mengi nyumbani utaisaidia Yanga Misri - Kiemba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Oct 2019
Ushindi wa mabao mengi nyumbani utaisaidia Yanga Misri - Kiemba

Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Amri Kiemba amesema njia pekee ya Yanga kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho, ni kuhakikisha wanapata ushindi mnono nyumbani

Oktoba 27 Yanga itashuka dimba la CCM Kirumba kumenyana na Pyramids Fc kutoka Misri ukiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi

Kiemba amesema mara nyingi timu za Tanzania huwa zinapata matokeo dhidi ya timu za Kaskazini katika michezo inayopigwa nyumbani lakini matokeo hayo mebamba huwa hayazisaidii kwenye michezo ya ugenin

Aidha Kiemba amesema licha ya Pyramids Fc kuwa timu isikuwa na uzoefu wa michuano ya CAF hii ikiwa mara yao yakwanza kushiriki, bado itakuwa timu hatari kwa Yanga kutokana na uwekezaji mkubwa wa timu hiyo na ubora wa ligi yao

"Naiangalia mechi hiyo kwa namna nyingine.Β  Kwa tofauti ya ligi ya Tanzania na Misri naona bado ni timu ngumu haijalishi tunacheza na timu gani. Tusiangalie historia ya timu tu, tuangalie pia historia ya ligi wanayocheza. Mechi haitakuwa rahisi," amesema

"Mara nyingi timu za Tanzania zimekuwa na uwezo wa kupata matokeo hata kwa timu za Afrika ya Kaskazini (kwenye mechi za nyumbani) shida imekuwa mechi inapokuwa ugenini."

"Tumeshindwa pia kupata magoli ya kutosha hapa nyumbani ili yazisaidie timu zetu ugenini. Ukishinda goli 1-0 nyumbani kwa timu za Kaskazini mwa Afrika unakuwa kama tayari umeshatoka."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’