Kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids, uongozi wa klabu ya Yanga umepania kuhamasisha mashabiki kuujaza uwanja wa CCM Kirumba
Uwanja huo unachukua mashabiki takribani 40,000
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema watahakikisha mashabiki wengi wanajitokeza CCM Kirumba Oktoba 27
Mayay apongeza
Naye mjumbe wa Kamati ya Ufundi Ally Mayay amepongea uamuzi wa Yanga kuupeleka mchezo huo jijini Mwanza akiamini uamuzi huo utaongeza hamasa kwa mashabiki kujitokeza CCM Kirumba tofauti na mchezo huo kama ungepigwa jijini Dar es salaam
Mayay ameeleza kuwa pindi Yanga wanapocheza katika dimba la Taifa kwa miaka ya hivi karibuni, hamasa ya mashabiki imekuwa chini
"Ni jambo zuri kwa sababu kuna uwezekano Yanga ikapata mashabiki wengi zaidi tofauti na Uwanja wa Taifa ambao umekuwa haupati watu wengi kwa miaka ya hivi karibuni;" amesema
"Uzuri wa kanda ya ziwa ni kuwa idadi ya mashabiki kutoka Shinyanga, Mwanza na hata Mara wanaweza wakasafiri kwenda Kirumba sababu si mbali"