CAF yathibitisha Molinga, Mustafa ruksa kuivaa Pyramids Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2019
CAF yathibitisha Molinga, Mustafa ruksa kuivaa Pyramids Fc

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limewatoa hofu viongozi wa klabu ya Yanga kuwa wataruhusiwa kuwatumia wachezaji wao David Molinga na Mustafa Suleyman kwenye mchezo wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc

Baada ya kuchelewa kupata vibali vya wachezaji hao, Uongozi wa Yanga uliiandikia barua CAF kutaka ufafanuzi wa suala hilo

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Rodgers Gumbo amesema CAF wamejibu barua hiyo ambapo wamewahakikishia kuwa wachezaji hao wataruhusiwa kucheza mechi ya Oktoba 27 na leseni zao zitatumwa kabla ya mchezo huo

Molinga amekuwa katika kiwango kizuri cha kupachika mabao, anaweza kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji kwenye mchezo huo

Aidha bado haijafahamika kama mkongwe Kelvin Yondani atapona majeraha kwa wakati na kuwahi mechi hiyo itakayopigwa Jumapili Oktoba 27

Ikumbukwe Yanga pia inaweza kumkosa beki wake Lamine Moro ambaye alionyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United nchini Zambia

Mustafa Suleyman anaweza kuwa mbadala wa Lamine

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’