Baada ya kuthibitisha kuwa mchezo wa kuwania nafasi ya kutinga makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc utapigwa Mwanza, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwasili jijini humo Oktoba 20
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema wanahitaji kufanya maandalizi mapema ili kuhakikisha wanashinda
"Mapema tu tarehe 20 mimi (Ten), Antonio Nugaz (Msemaji na Mhamasishaji) pamoja na Mkuu wa idara ya Habari Hassan Bumbuli, tutakuwa tushatua Mwanza kwa ajili ya maandalizi na mikakati chanya ya kupata ushindi mkubwa siku ya mchezo," amesema
Aidha, Ten amewahakikishia wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga kuwa lengo lao ni kushinda Oktoba 27 hivyo watafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo
Mchezo huo wa kukata na shoka, utapigwa saa kumi kamili jioni
Yanga imejipanga kwelikweli kuelekea mchezo huo. Suala la kuweka mazingira yatakayo wanufasha nyumbani ni jambo la msingi
Waarabu sio kwamba wanakuwa na timu nzuri sana, lakini wanapokuwa nyumbani si rahisi kuwafunga kwa sababu wanafanya maandalizi ya ndani na nje ya uwanja
