Tarehe kama ya leo alizaliwa mlinda lango wa Yanga Farouk Shikalo
Shikalo ametua Yanga usajili wa msimu huu akitokea klabu ya Bandari Fc
Baada ya kumkosa kwenye usajili wa dirisha dogo mwaka jana, hatimaye Yanga ikafanikiwa kuinasa sahihi yake kule nchini Misri wakati akishiriki michuano ya Afcon akiwa na Harambee Stars
Hakuna mwenye mashaka na uwezo wake, kwani tayari amedhihirisha kwa nini kocha Mwinyi Zahera alihitaji sana sahihi yake ili kumaliza changamoto ya walinda lango ambayo iliitesa Yanga misimu miwili iliyopita
Pamoja nae, siku kama ya leo pia alizaliwa kiungo kiraka, Mapinduzi Balama
Msimu huu Yanga inajivunia kuwa na nyota hawa ambao kazi yao dimbani imeanza kuwa na manufaa kwa timu

Tunawatakia kila la kheri katika siku hii muhimu kwao
Happy BirthDay wapambanaji