Ili kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa ni lazima kuwa na mkakati wa ushindi. Yanga imekuja na mkakati wa ushindi baada ya kocha Mwinyi Zahera kupendekeza mchezo dhidi ya Pyramids Fc ukapigwe uwanja wa CCM Kirumba
Miaka ya nyuma Yanga ilikuwa ikitumia uwanja wa CCM Kirumba kwenye mechi kubwa na ilifanikiwa kushinda mechi nyingi zilizochezwa kwenye uwanja huo
Inaelezwa Zahera ametoa maelekezo kwa viongozi wa Yanga kuhakikisha mchezo dhidi ya Pyramids unapelekwa Kirumba
Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc jijini Mwanza kabla ya kuwakabili Pyramids Fc Oktoba 27
Inatarajiwa kuelekea jijini Mwanza Oktoba 20
ADVERTISE HERE