Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' hakusafiri na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho tayari kimewasili Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki
Fei Toto amesema ameshindwa kusafiri kutokana na hati yake ya kusafiria kuisha muda
Fei Toto atakosa mchezo huo wa kirafiki ambao utapigwa Oktoba 14 Kigali, Rwanda na mchezo dhidi ya Sudan ambao utapigwa Oktoba 18 nchini Uganda
Aidha beki kisiki Kelvin Yondani nae hakusafiri kwa kuwa ni majeruhi
Mlinda lango Metacha Mnata na Abdulaziz Makame ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa kwenye kikosi hicho
ADVERTISE HERE