Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema hawahofii kupangwa na Pyramids Fc kwa kuwa walijiandaa kukutana na timu yoyote kwenye hatua ya mtoano
Mwandila aliyeachiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga baada ya kocha Mkuu Mwinyi Zahera kurejea DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa, amesema wanajiandaa kikamilfu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
"Timu zote zilizofika hatua hii ni nzuri, tutajiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo bora, hatuwezi kurekebisha historia ya nyuma, lakini tunaweza kujiandaa kuweka historia mpya ya baadaye," amesema Mwandila
Kikosi cha Yanga kilianza rasmi maandalizi kuelekea mchezo huo juzi, kesho kikitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers
Inaelezwa mchezo huo utakuwa wa ndani, hautarushwa mbashara kwa kuwa ni sehemu ya program ya mazoezi iliyoachwa na Zahera