Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu na kombe la Shirikisho, Yanga itacheza mechi mbili za kirafiki
Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema, Jumamosi Oktoba 12 Yanga itacheza na Friends Rangers na mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Pan Africans Oktoba 18
Oktoba 20 Yanga itaelekea mkoani Mwanza tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 24 na baadae Yanga kurejea jijini Dar es salaam kuisubiri Pyramids FC
ADVERTISE HERE