Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mshambuliaji wa timu hiyo David Molinga ataweza kucheza mchezo wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc Oktoba 27
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Molinga na Mustafa Suleyman hawakuwa na vibali vya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua za mwanzo kwa kuwa walipaswa kupata vibali baada ya Septemba 30
Bumbuli amesema wana uhakika vibali vyao vitawasili wakati wowte na wataweza kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Pyramids itakayopigwa Oktoba 27 uwanja wa Taifa
Kuongezeka kwa Molinga kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ni habari njema kuelekea mchezo huo kwani Mcongomani huyo kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga
ADVERTISE HERE