Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc
Mchezo huo utapigwa Oktoba 22 jijini Mwanza
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema timu itandelea kujifua uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam
Aidha Mwakalebela amesema huenda timu itacheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuelekea Mwanza
Yanga inakabiliwa na michezo miwili ya ligi kuu kanda ya ziwa kwani baada ya kucheza na Alliance Oktoba 22, Oktoba 26 itacheza na Mbao Fc michezo yote ikipigwa uwanja wa CCM Kirumba
ADVERTISE HERE