Droo mchujo kombe la Shirikisho itafanyika leo nchini Misri Hoteli ya Hilton Pyramids Resort iliyopo jijini Cairo kuanzia saa 2:00 Usiku
Katika droo hiyo, Yanga itakuwa kwenye chungu kimoja sambamba na timu nyingine 15 zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku chungu kingine kikiwa na timu 16 zilizotinga hatua ya mchujo ya Kombe la Shirikisho ambapo zitakutanishwa pamoja kusaka klabu 16 zitakazotinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho msimu huu.
Timu 16 Kombe la Shirikisho ambazo zimetinga hatua ya mchujo ya mashindano hayo ni RS Berkane. (Morocco),Al-Masry (Misri),Hassania Agadir (Morocco), Zanaco (Zambia), Enugu Rangers (Nigeria ), Djoliba (Mali), Paradou AC (Algeria), ESAE (Benin), DC Motema Pembe (DR Congo), FC San Pedro (Ivory Coast), Pyramids (Misri), Bandari (Kenya), Bidvest Wits (Afrika Kusini), TS Galaxy (Afrika Kusini), Proline (Uganda) na Triangle United (Zimbabwe).
Ukiachilia mbali na Yanga, timu nyingine 15 zilizoondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni UD Songo (Msumbiji), Cote d'Or (Shelisheli), Green Eagles (Zambia), Fosa Juniors (Madagascar), Elect-Sport (Chad), KCCA (Uganda), Asante Kotoko (Ghana), FC Nouadhibou (Mauritania), Cano Sport (Guinea ya Ikweta), Gor Mahia (Kenya), ASC Kara (Togo), Horoya (Guinea) na Al Nasr (Libya).
Droo hiyo itarushwa mbashara kupitia runingani, DSTV kupitia Supersport 9 watakuwa mbashara kuanzia saa mbili usiku