Viongozi Yanga wafarijika kuachiwa Manji

Mwana Jangwani By Mwana Jangwani
•
7 Oct 2017
Viongozi Yanga wafarijika kuachiwa Manji
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha, jana Ijumaa hata kabla wikiendi haijaanza alimwachia huru mwanachama tajiri wa Yanga, Yusuf Manji, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka la kutumia dawa za kulevya.

“Kusema ukweli nimefarijika sana kwa Manji kuachiwa huru kwa sababu mimi ndiye niliyemuwekea dhamana,” alisema Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa mara baada ya Manji kutoka mahakamani hapo.

“Katika kipindi chote nilikuwa na wasiwasi kuwa pengine lolote linaweza kutokea, lakini nashukuru Mungu ameachiwa huru.”

Mkwasa aliyewasili mahakamani akiambatana na baadhi ya wanachama, viongozi na mashabiki wa klabu hiyo aliongeza: “Tunaomba aje uraiani, tushirikiane katika majukumu.”

Wakili wa Manji, Hajra Mungula alisema: “Hukumu imetolewa vizuri na kama kuna lolote litasemwa baadaye.”

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ameshindwa kumtia hatiani mshtakiwa hivyo anamuachia huru.

Katika kesi hiyo, Manji alidaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin. Akipitia baadhi ya ushahidi mahakamani hapo, Hakimu Mkeha alisema shahidi wa tatu ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) alidai anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusufali Manji (41) kuwa na vyuma vinne kwenye moyo.

Awali, Yusuf Manji alidai kuwa yeye ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka kwa babu zake ambao walikwishafariki kwa ugonjwa huo.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →