Majukumu ya Zahera DR Congo yanavyoiathiri Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
8 Oct 2019
Majukumu ya Zahera DR Congo yanavyoiathiri Yanga

Wakati wa michuano ya Afcon mdau mmoja aliweka makala humu ndani akionyesha hofu yake kwa Yanga kuanza maandalizi ya msimu mpya bila ya kuwa na kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera ambaye alikuwa Misri na timu ya Taifa ya DR Congo akishiriki michuano ya Afcon

Pengine kwa kiasi fulani, maandalizi ya Yanga mwanzoni mwa msimu yaliyumba baada ya kocha huyo kuchelewa

Kutokana na kikosi cha Yanga kuwa na nyota wengi wapya, ilipaswa Zahera mwenyewe aifanye kazi ya kukiandaa kikosi chake tangu mwanzo

Bado changamoto hiyo itaendelea kuiathiri Yanga kwa kiasi fulani kama uongozi hautakaa chini na Zahera kuliweka jambo hili sawa

Mwishoni mwa mwezi huu Yanga inakabiliwa na mchezo muhimu wa kombe la Shirikisho ambao matokeo ya ushindi yanaweza kuwaweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho

Lakini pia Oktoba 22 Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc

Sasa kulingana na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga Hassani Bumbuli, Zahera amerejea DR Congo kutekeleza majukumu ya timu ya Taifa

Anatarajiwa kurudi nchini Oktoba 19, siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Alliance na wiki moja kabla ya mchezo wa kombe la Shirikisho

Viongozi wa Yanga wanapaswa kuliangalia hili kwa mapana ili kocha huyo apewe mkataba ambayo utamuondolea majukumu ya timu ya Taifa angalau kwa muda ili ajikite katika kuijenga Yanga

Licha ya kuandaa program ya mazoezi na kumuachia Mwandila, lakini naamini mafanikio zaidi yangepatikana kama angesimamia mazoezi hayo yeye mwenyewe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’