Baada ya kujiengua kwa aliyekuwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya DR Congo Florent Ibenge, mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera ameendelea kuaminiwa nchini humo sasa akitarajiwa kuiongoza timu hiyo katika mechi mbili za kirafiki akishirikiana na Mihayo Kazembe, kocha wa TP Mazembe
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa Zahera ameenda DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa na atarejea nchini Oktoba 19
Wakati wote ambao atakosekana timu itakuwa chini ya Noel Mwandila
Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku tatu na wanatarajiwa kurejea mazoezini kesho Jumatano kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa Oktoba 22
Aidha ratiba inaonyesha, Oktoba 26 Yanga inapaswa kucheza na Mbao FC hukohuko jijini Mwanza hata hivyo mchezo huo huenda ukaahirishwa kwani Oktoba 27 Yanga itacheza mechi ya kwanza ya mtoano kombe la Shirikisho jijini Dar es salaam