Stars yaikabili Malawi leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
7 Oct 2017
Stars yaikabili Malawi leo
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Jumamosi kinashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh 3,000 na kikubwa ni Sh 5,000.

Kuelekea mchezo huo, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, amesema wana uhakika wa kushinda leo kutokana na maandalizi waliyofanya kambini.

Mchezo huo ambao upo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), unatolewa macho na timu zote mbili kama sehemu ya kujiandaa na mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika 2019.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Malawi, Ronny van Geneugden, amesema: “Tanzania tunaifahamu ni timu nzuri na inatoa ushindani ukikutana nayo, tulikutana nayo katika Cosafa Cup naamini ni kipimo
kizuri kwetu.”

Naye Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema: “Vijana wangu wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo), kikosi hiki kitanipa taswira ya timu
yetu ambayo inaelekea kucheza mechi za kufuzu Afcon 2019.”

Nahodha Samatta aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao huku akisema mchezo huo una umuhimu kwao kujitengenezea nafasi ya kupanda kwenye viwango vya Fifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →