Uongozi wa klabu ya Yanga umewapa siku tatu za mapumziko wachezaji wa timu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu itarejea kuanza mazoezi Oktoba 09 kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa Oktoba 22 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Katika hatua nyingine, Bumbuli amesema kocha Mkuu Mwinyi Zahera anaondoka nchini kuelekea DR Congo kuiongoza timu ya Taifa ya nchi hiyo katika michezo miwili ya Kimataifa ya kirafiki
Zahera anatarajiwa kurejea Oktoba 19 kuendelea na majukumu yake katika kikosi cha Yanga
ADVERTISE HERE