Beki Ali Ali amekuwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga hasa anapocheza beki ya kulia
Lakini anakuwa mchezaji tofauti anapokuwa anacheza safu ya ulinzi wa kati
Jana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alikuwa muhimili imara wa Yanga
Pamoja na kuwa wakati mwingine hufanya makosa yasiyotarajiwa, Ali ni mzuri anapocheza nafasi ya ulinzi wa kati kwani ana utulivu wa hali ya juu
Mwili wake unaonekana mdogo lakini ukizungumzia mabeki mahiri wa kucheza mipira ya vichwa yeye anaweza kuwa namba moja Tanzania
Wakati mwingine unaweza ukaelewa kwa nini Yanga haina presha ya kum-bembeleza beki Andrew Vicent aliyegoma kwa kuwa wanaye Ali Ali
Dante naye ni hodari wa kucheza mipira ya juu lakini huyu Ali Ali ni zaidi yake linapokuja suala la mipira ya vichwa
Jana alichangia kupatikana kwa bao la Yanga, pasi yake ya kichwa kwa Makame ilizaa bao la ushindi kwa mabingwa hao wa kihistoria