Kitu pekee ambacho wachezaji wa Yanga wanafikiria ni kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union kesho
Mchezo huo wa tatu kwa Yanga msimu huu, utapigwa uwanja wa Uhuru
Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na kisha kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania juzi, ushindi ndio matokeo pekee ambayo yatarejesha morali ya mashabiki
Kiungo Abdulaziz Makame amesema matokeo ya sare waliyopata dhidi ya Polisi Tanzania yamewaumiza sana wachezaji na wamepania kushinda kesho
"Kuwa na alama moja baada ya michezo miwili ni jambo linalotuumiza sana. Tutahakikisha tunashinda mchezo wa Jumapili ili kuwapa furaha mashabiki wetu ili waendelee kutuunga mkono," amesema
"Ligi ni ngumu, timu zote zimejipanga lakini baada ya kuteleza michezo miwili, tunahitaji kufanya vizuri michezo yote iliyobaki"
"Coastal Union sio timu mbaya lakini jambo pekee tunalohitaji kwenye mchezo huo ni ushindi"
Kiingilio cha mchezo huo ni Tsh 15,000/- VIP na Tsh 5,000/- Mzunguuko