Beki wa kulia Juma Abdul leo amepata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Polisi Tanzania
Huo utakuwa mchezo wa kwanza kwa Abdul kucheza msimu huu
Mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku ya kumuona dimbani fundi huyo wa kumimina majaro
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo amewaanzisha washambuliaji wake tegemeo David Molinga, Juma Balinya na Sadney Urikhob ambaye atashambulia akitokea winga ya kushoto
Winga Patrick Sibomana na nahodha Papy Tshishimbi wamekosa mchezo huo kwa kuwa ni majeruhi
Aidha Zahera pia amempa nafasi Mrisho Ngasa winga ya kulia wakati Fei Toto na Makame wanaendelea kucheza pamoja sehemu ya kiungo
Safu ya ulinzi ni ile ile iliyocheza dhidi ya Zesco, mabadiliko pekee akiwa Abdul aliyechukua nafasi ya Ally Ally