Mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amesema ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania, utakuwa silaha muhimu ya kuwanyamazisha wakosoaji wao
Jioni ya leo Yanga itashuka dimba la Uhuru kucheza mchezo wake wa pili wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Polisi inayonolewa na kocha Selemani Matola
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Balinya amesema leo wanahitaji kushinda
"Ni jambo la kawaida timu inapokuwa haipati matokeo, yapo mengi yatasemwa lakini njia ya kutuliza hali hiyo ni ushindi," amesema
"Tunafahamu tunahitaji matokeo leo ili kuwapa furaha mashabiki wetu lakini pia kuwanyamazisha wale wasiotupenda"
"Tulipoteza mchezo wa kwanza, hatuko tayari kupoteza mchezo wa pili mfululizo"
Yanga imeuchukulia mchezo huo kwa uzito mkubwa
Mabingwa hao wa kihistoria waliingia moja kwa moja kambini baada ya kurejea kutoka Zambia