Ngorongoro Heroes imetinga fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 inayofanyika nchini Uganda baada ya kuichapa Sudan mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali
Mabao ya Kelvin John 'Mbappe' na Israel Mwenda yalitosha kuihakikishia Tanzania ushindi muhimu dhidi ya Sudan ambayo bao lake pekee kwenye mchezo huo lilifungwa Mohammed Abbas
Tanzania sasa itacheza fainali dhidi ya Kenya baada ya timu hiyo kuichapa Eritrea bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali
Mchezo wa fainali utapigwa Oktoba 06
Hongera vijana wa Tanzania kwa mafanikio hayo Uganda
ADVERTISE HERE