Yanga yahitaji miezi mitatu kukamilisha uwanja wa Kaunda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2019
Yanga yahitaji miezi mitatu kukamilisha uwanja wa Kaunda

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa ukarabati wa uwanja wa Kaunda unaendelea ambapo mkapa kufikia February 2020 utakuwa umekamilika

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema zoezi la kujaza kifusi limekamilika, kazi inayofanyika sasa ni usambazaji wa kifusi hicho tayari kuanza zoezi la kupanda nyasi

"Tunaendelea na ujenzi wa uwanja wetu wa Kaunda ambao hivi sasa upo kwenye hatua ya kusawazazishiwa udongo, kuna greda mbili ambazo zinafanya kazi hiyo," amesema

"Baada ya kusawazisha udongo huo, zoezi litakalofuata ni kuweka udongo mwingine ambao ni wa rutuba kisha upandaji wa nyasi utafuatia, na mpaka kufikia raundi ya pili ya ligi unaweza kuwa umekamilika"

Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa,  kutokana na ukubwa wa eneo hilo, watatoa viwanja viwili, kimoja cha nyasi bandia na kingine cha nyasi asili

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa Kigamboni, Mwakalebela amesema mchakato inaendelea ambapo kuna Kamati maalum imeundwa kusimamia zoezi la hilo

Jana Yanga iliweka hadharani wajumbe wa Kamati hiyo inayosimamia masuala yote ya ujenzi na Miundombinu

Kukamilika kwa uwanja wa Kaunda kutaipunguzia timu hiyo gharama za kukodi viwanja

Yanga imekuwa ikifanya mazoezi uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’