Singida United yaipiga mkwara Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
6 Oct 2017
Singida United yaipiga mkwara Yanga
Singida United imeanza kuitishia nyau Yanga baada ya kusema kuwa, mabingwa hao watetezi waanze kujiandaa kisaikolojia kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi yao, mchezo uatakaopigwa Novemba 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Namfua Singida.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amesema kuwa, Yanga wanahitaji kujiandaa kisaikolojia kabla ya mchezo huo kwani watakuwa wametoka kwenye mechi ngumu dhidi ya Simba na wanakwenda kukutana nao.

Alisema, mechi hiyo ya kwanza kwao katika Uwanja huo ambao haujatumika tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu kutokana na kuwa katika ukarabati, wanajiandaa kuonyesha soka safi mbele ya mabingwa hao watetezi lakini pia kwa mashabiki wa timu hiyo mkoani humo.

Singida kwa sasa wanatumia Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani ambapo kwa sasa wapo katika maandalizi yake kuelekea mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting, Oktoba 14 mwaka huu.

Timu hiyo inatarajiwa kuwafuata Ruvu, Oktoba 12 mwaka huu kwenda Pwani kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mabatini Pwani.

“Timu ipo katika hali nzuri, tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Ruvu, lakini baada ya hapo tutakwenda kucheza na Ndanda kabla ya kuwavaa Mtibwa Sugar ambapo kote wanahitaji kukusanya jumla ya pointi tisa kwenye mechi hizo zote.

“Baada ya mechi hizo, tunarudi kwenye Uwanja wetu wa nyumbani wa Namfua, Singida kucheza na Yanga, mchezo utakuwa na ushindani wa hali ya juu kwani tunahitaji kuonyesha soka la hali ya juu hivyo wapinzani wetu wajiandae kisaikolojia,” alisema Sanga.

Timu hizo zilikutana wakati wa maandalizi ya msimu mpya kwenye mchezo wa kirafiki ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →