Baada ya kumaliza majukumu ya ligi ya mabingwa keshokutwa Alhamisi Yanga inarejea kwenye mikikimikiki ya ligi kuu ya Vodacom ikiikaribisha Polisi Tanzania kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono wachezaji wao
Kiingilio cha chini ni Tsh 5,000/- Mzunguuko na VIP ni Tsh 15,000/-
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo hasa ikizingatiwa ilipoteza mchezo wa ufunguzi kwa kufungwa na Ruvu Shooting bao 1-0
ADVERTISE HERE