Ni dhahiri Yanga bado haitaweza kuwatumia wachezaji wake wawili Mustafa Suleyman na David Molinga kwenye mchezo wa mtoano kusaka nafasi ya kutinga makundi kombe la Shirikisho
Wachezaji hao hawakupata leseni kutoka CAF baada ya kuchelewa kupatikana kwa ITC zao
Msimu huu CAF iliweka vipindi tofauti vya kukamilisha usajili wa wachezaji ili waweze kucheza kuanzia hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho
Kwa wachezaji ambao usajili wao ulikamilishwa awamu ya mwisho wataruhusiwa kutumika kuanzia hatua ya makundi
Inavyoonekana Molinga na Mustafa hawakupata leseni kwa kuwa usajili wao ulifanyika kwenye awamu ya mwisho ambapo pia iliilazimu Yanga kulipa faini ili kuweza kuwaandikisha
Hivyo wachezaji hao wataweza kuichezea Yanga kuanzia hatua ya makundi kama itafuzu