Makame awaomba radhi mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2019
Makame awaomba radhi mashabiki Yanga

Kiungo wa Yanga, Abdulaziz Makame ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo, baada ya juzi kujifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Mchezaji huyo alisema tukio hilo ni baya zaidi kutokea kwake tangu alipoanza kucheza soka.

Akizungumza jana, Makame amewataka mashabiki kusahau bao hilo na kujiandaa vyema kwa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Makame aliyecheza kwa kiwango bora katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini, alijifunga bao dakika ya 78 katika harakati ya kuokoa kiki ya mpira wa krosi iliyopigwa upande wa kushoto na winga Quadri Aladeokun.

Akizungumzia bao hilo, Makame alisema lengo lake lilikuwa kutoa mpira nje baada ya kuona anakabiliwa na wachezaji wawili wa Zesco nyuma yake.

"Nilikwenda kasi kuzuia mpira baada ya kuona nyuma yangu kuna wachezaji wa Zesco, nikiwa na uhakika wa kutoa nje bahati mbaya nikajifunga,"alisema Makame.

Kiungo huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Mafunzo ya Zanzibar, alisema kilichotokea ni sehemu ya mchezo na amewataka wadau wa klabu hiyo kujipanga kwa Kombe la Shirikisho.

Makame alisema Yanga inapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kwa kuwa mashindano hayo yanashirikisha timu zenye uzoefu, hivyo wanapaswa kujiandaa kikamilifu.

Kiungo huyo alikuwa nyota wa mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam waliotoka sare ya bao 1-1.

Baada ya mchezo huo, Kocha wa Zesco, George Lwandamina alisema Makame ni mchezaji wa aina yake na alikuwa kikwazo kwa timu yake kupata ushindi.

Lwandamina alisema tukio la kujifunga linaweza kumpata mchezaji yeyote na sehemu ya mpira.

"Ni tukio la bahati mbaya yule kijana ni hodari sana katika nafasi ya kiungo"

"Jambo hili lingeweza pia kumpata mchezaji wangu. Lakini wenye nafasi ya kumjenga au kumbomoa ni wachezaji wenzake na benchi la ufundi la Yanga kwa namna watakavyopokea tukio lile," alisema Lwandamina.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’