Tunahitaji kufunga mabao mengi nyumbani - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2019
Tunahitaji kufunga mabao mengi nyumbani - Zahera

Baada ya Yanga kuondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa na kushushwa kombe la Shirikisho, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema ili kuwa na uhakika wa kutinga makundi watahitaji kufunga mabao mengi nyumbani

Zahera ambaye timu yake iliondolewa na Zesco kwa kufungwa mabao 2-1, amekiri kuwa uhaba wa mabao nyumbani umewasababishia kushindwa kuingia makundi ligi ya mabingwa

"Hakufunga mabao mengi, tulikuwa na changamoto za hapa na pale kwenye safu yetu ya ushambuliaji lakini sasa nadhani tumeanza kuwa vizuri," amesema

"Hatupaswi kurudia makosa tuliyofanya ligi ya mabingwa, tunahitaji kufunga mabao zaidi ya mawili nyumbani ili kupunguza presha ya mchezo wa ugenini"

Yanga inasubiri kumjua mpinzani wake droo ikitarajiwa kufanywa wiki ijayo nchini Misri

Jambo la uhakika ni kuwa Yanga itaanzia nyumbani na baadae kwenda kumalizia ugenini

Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa beki wake kisiki Lamine Moro aliyepewa kadi mbili za njano kwenye mchezo dhidi ya Zesco

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’