CAF hutoa nafasi 4 za ushiriki wa vilabu kwa kila nchi miongoni zile 12 bora barani Afrika.
Ubora wa kila nchi hupimwa kwa mafanikio ya vilabu vyake kwenye mashindano ya Afrika; Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Tanzania ni ya 12 ikiwa na pointi 18 ilizovuna kutokana na mafanikio ya Yanga na Simba katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Yanga iliingia mara 2 hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, 2016 na 2018. Hatua kama hiyo huipatia nchi husika pointi 2.5. Hivyo pointi 2.5 za 2016 na 2018 kutoka kwa Yanga zikaipatia Tanzania jumla ya pointi 5.
Simba ikaingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa 2018/19. Hatua kama hiyo huipatia nchi husika pointi 15.
Kwa hiyo, Tanzania ilistahili iwe na pointi 20 jumla, yaani 5 za Yanga na 15 za Simba.
KWANINI HAZIPO?
Kiutaratibu, CAF hupima viwango vyao kwa mafanikio ya ndani ya kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Kila mwaka mmoja unapoongezeka, thamani ya pointi za mwaka wa nyuma zaidi hupungua.
Kwa mafanikio ya Simba, 2018/19, hesabu zake za miaka 5 zilianzia 2015.
Hivyo, pointi 5 za Yanga zilipungua thamani mwaka 2019, na kubaki 3 na zilipojumlishwa na zile 15 Simba za 2018/19, ndiyo zikawa 18.
HATARI YAKE
Kutokana na utaratibu huo, msimu ujao wa mashindano ya Afrika, 2010/21, Tanzania itabaki na pointi 17 kwa sababu zile 3 za Yanga, zitabaki.
Kwa maana hiyo, hatari ya Tanzania kupoteza nafasi 4 za ushiriki ni kubwa mno, endapo... YANGA HAWATOFIKA HATUA YA MAKUNDI YA SHIRIKISHO
Watanzania tuungane kama taifa kwa maombi na jitihada zozote zile ili kuisaidia Yanga ivuke hatua ya mchujo ya Kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya makundi.
Hii itaipatia Tanzania pointi 2.5 ambazo zitaongezwa na 17 zitakazobaki na kuwa 19.5.
Na kama Yanga itafanikiwa kushika nafasi ya 3 katika kundi lake, Tanzania itapata pointi 5, hivyo tutakuwa na pointi 22. Na kama ikifika robo fainali, itaipatia Tanzania pointi 10, zikiongezwa na 17, tutakuwa na pointi 27. Hapo nafasi yetu itakuwa salama salmini.
CC : @zakazakazi