Tukio la Abdulaziz Makame kujifunga kwenye mchezo dhidi ya Zesco limeendelea kumtesa kiungo huyo ambaye pengine anahitaji kusaidiwa kisaikolojia ili kweza kurudi katika hali ya kawaida
Lakini kimsingi ni tukio la bahati mbaya, hapaswi kulaumiwa
Matukio hayo huwatokea wachezaji wote
Makame ni mchezaji aliye kwenye kiwango cha juu sana sasa
Mchango wake kwenye kikosi cha Yanga unaonekana waziwazi
Makame aliwapa wakati mgumu Zesco katika michezo yote miwili jijini Dar es salaam na jana Zambia
Anastahili pongezi kwa kazi kubwa anayofanya dimbani
Tukio la jana halipaswi kumfanya ajione mnyonge au kutupiwa lawama kwani ilikuwa bahati mbaya
Afisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amemtaka kiungo huyo asahau kilichotokea
"Wewe ni fundi wa mpira na Makosa ni sehemu ya matokeo ya mpira wenyewe,usiyumbe Wala Usijali Endelea kupambana tu..sisi hatuna Neno na wewe uwezo wako unaonekana tunauthamini"