Ligi Kuu ya Vodacom imeingia raundi ya tano leo kwa mechi tano kupigwa katika viwanja mbalimbali
Jijini Dar es salaam KMC imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda Fc, matokeo kama hayo ikipata Mtibwa Sugar dhidi ya Mbeya City
Lipuli Fc pia imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Tanzania Prisons wakati Kagera Sugar ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka JKT Tanzania
Nayo Biashara United ambayo juzi ilimtimua kocha wake Amri Said kutokana na matokeo mabaya msimu huu, imefungwa mabao 2-0 na Simba
Biashara United imefungwa michezo minne kati ya mitano waliyocheza mpaka sasa
Wakati ligi hiyo ikiendelea kuchanja mbuga, Yanga itarejea dimbani katikati ya wiki kuikabili Polisi Tanzania
Yanga itahitaji kushinda michezo yake ya viporo ili kwenda na kasi ya watani zao Simba ambao wameshinda michezo yote minne ya kwanza wakifikisha alama 12
Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting, ushindi katika mchezo unaofuata ni matokeo ya lazima kwa kikosi cha kocha Mwinyi Zahera