Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kitakachoikabili Zesco United baadae
Hii ni kutokana na kikosi chake alichopanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam na kulazimishwa sare ya bao 1-1 kufanya vizuri
Mlinda lango Metacha Mnata anatarajiwa kulindwa na safu aliyoanza nayo mchezo wa kwanza
Pengine nafasi ambayo itakuwa na mabadiliko ni upande wa kulia
Kiraka Mapinduzi Balama hakusafiri na timu baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa kwanza
Pengine Juma Abdul anaweza kuaminiwa akaanza katika nafasi hiyo
Mabadiliko mengine yanaweza kuwa kwenye safu ya ushambuliaji ambapo Juma Balinya huenda akarejeshwa kikosini
Kati ya Feisal Salum au Mohammed Issa 'Banka' mmoja huenda akaanzia benchi wakati Makame na Tshishimbi wakiwa na uhakika wa kuanza leo kutokana na mchezo mzuri waliokuwa nao katika mchezo wa kwanza
Zahera anaweza kutumia mfumo wa 4-4-2/4-3-3 kama alivyocheza nchini Botswana alipokwenda kuikabili Township Rollers
Kikosi kinachotabiriwa:
Metacha, Abdul, Sonso, Lamine, Yondani, Makame, Banka/Feisal, Tshishimbi, Sadney, Balinya, Sibomana