Mwashiuya ndiye 'Msuva' aliyebakia Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Oct 2017
Mwashiuya ndiye 'Msuva' aliyebakia Yanga
Licha ya kukaa nje kwa wiki kadhaa kutokana na majeruhi, winga Geogrey Mwashiuya ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Yanga ambao viwango vyao viko juu.

Yanga imeanza kwa kusuasua msimu huu lakini niwaambie moja ya sababu ni kwamba baadhi ya wachezaji wakongwe bado hawajafikia viwango vyao vya msimu uliopita.

Lakini si kwa Mwashiuya, ambaye baada ya kurejea kutoka kwenye majeruhi ameuanza msimu kama alivyoumaliza msimu uliopita.

Aidha, viwango vilivyoonyeshwa na Gadiel Michael, Mwashiuya, Buswita na Ajib katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar vinaashiria kuwa Yanga bado inaweza kucheza 'attacking football'.

Miaka yote Yanga imekuwa ikishambulia kupitia pembeni ikiwatumia mawinga wake wenye kasi na umahiri wa kupiga krosi.

Mfumo huo umeshindwa kutumika katika michezo ya mwanzoni mwa msimu baada ya 'kukosekana' wachezaji hivyo kuifanya Yanga ipate wakati mgumu kwenye kupachika mabao.

Kuumia kwa Mwashiuya na Baruani Yahya ambaye hata hivyo bado anahitaji muda aweze kuvivaa viatu vya Msuva, kuliifanya Yanga ikose winga wa asilia hivyo kuwatumia wachezaji ambao hawakuzoea kucheza pembeni.

Ndio, Yanga ina vijana wengi wanaoweza kucheza pembeni lakini ni wazi viwango vyao vinatofautiana kwa kuwa kila mmoja ana mapungufu yake.

Juma Mahadhi, Emanuel Martin na Yusuph Mhilu ni mawinga lakini licha ya kutumika kwenye michezo kadhaa wameshindwa kulishawishi benchi la ufundi kupata namba za kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Badala yake tumeona mara kadhaa wachezaji kama Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib wakipangwa pembeni licha ya kwamba kwa asili hawa ni washambuliaji wanaomudu kucheza kati

Kwa sasa Mwashiuya anabaki kuwa moja ya silaha muhimu iliyobakia Yanga msimu huu baada ya kuondoka Saimon Msuva.

Mwashiuya kama hatakumbwa na majeraha ya mara kwa mara anaweza akaisaidia Yanga kurejesha ule mfumo wake wa kushambua kwa kasi kutokea pembeni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’