Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga keshokutwa Jumamosi watashuka uwanja wa Levy Mwanawasa kuikabili Zesco United katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wiki mbili zilizopita, Yanga ina kazi moja tu ya kusaka ushindi ili iweze kutinga hatua ya makundi
Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amesema wamekwenda Zambia kushinda mechi ili kujihakikishia tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Jambo hilo linawezekana hasa timu husika inapokuwa ni Yanga
Kwa Tanzania nadhani ni Yanga pekee ambayo ina rekodi nzuri inapocheza ugenini
Hivyo jambo kubwa kwa mashabiki ni kuwa na imani kwa timu yao kuwa inaweza kushinda Jumamosi
Morali ya wachezaji iko juu, kila mmoja ana shauku ya kushiriki hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Kwani wanafahamu, kwa kutinga hatua hiyo wanakuwa kwenye nafasi ya kujitangaza na pengine kusajiliwa na timu zenye maslahi zaidi
Hii ni mechi ambayo itakuwa kipimo sahihi cha uimara wa kikosi cha Yanga
cutIwapo Yanga itaiondosha Zesco, itadhihirisha kuwa ipo tayari kucheza na timu yoyote barani Afrika
Aidha itakuwa salamu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa mabingwa wa kihistoria wamerudi
Pia itakuwa ni heshima kubwa kwa kocha Zahera ambaye siku za karibuni baadhi ya mashabiki wameonyesha kukosa imani nae kutokana na matokeo yasiyoridhisha
Ushindi dhidi ya Zesco utafungua ukurasa mpya kwa kocha huyo, hata wale wanaomsema wataanza kumuheshimu
Wanayanga wameonyesha umoja kuelekea mchezo huo, kujitokeza kwa mashabiki wengi kwenda kuiunga mkono timu Zambia, inadhihirisha upendo wa mashabiki kwa timu yao