Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mabasi matano yanaelekea Zambia na mashabiki wa timu hiyo kuongeza nguvu katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United ambao utapigwa Jumamosi
Afisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema mabasi mengine yataanzia safari Mbeya na Tunduma
Mashabiki zaidi ya 300 wanahusika kwenye msafara huo ambao unatarajiwa kuwasili nchini Zambia kesho
Nugaz amesema ari ya timu iko juu, hamasa ya mashabiki ni kubwa na wana matumaini kuwa wanakwenda Zambia 'kuvunja mwisho' kw akuifunga Zesco United kwenye uwanja wake
ADVERTISE HERE