Sadney abeba matumaini ya Yanga Zambia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2019
Sadney abeba matumaini ya Yanga Zambia

Mshambuliaji Sadney Urikhob ni miongoni mwa wachezaji waliotangulia kwenye msafara wa kwanza wa kikosi cha Yanga ulioondoka mapema leo kuelekea Zambia tayari kwa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United

Sadney alisababisha mkwaju wa penati katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1

Ukiachana na changamoto ya kutofunga mabao, Sadney ni mchezaji anayejituma sana kwenye kikosi cha kocha Mwinyi Zahera

Zahera ameonyesha kuwa na imani nae akisisitiza kuwa wakati utafika atafunga mabao

Mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco utakaopigwa Septemba 28 huko Zambia, una umuhimu wa kipekee kwa Mnamibia huyo

Kwani kama ataisaidia Yanga kutinga hatua ya makundi atajijengea heshima mbele ya mashabiki ambao wameonyesha kutokuwa na imani nae

Lakini pia mafanikio katika mchezo huo yatamuongezea kujiamini na atafanya vizuri zaidi Yanga itakaporejea kwenye ligi

Ni hivyo hivyo kwa mshambuliaji Juma Balinya ambaye kocha Mwinyi Zahera huenda atamtumia Zambia

Balinya alikosa mchezo wa kwanza kutokana na changamoto ya kutokuwa fiti

Bila shaka kukaa kwake nje kulimpa nafasi ya kuwasoma walinzi wa Zesco na pengine atatumia udhaifu wao kuipa Yanga ushindi siku ya Jumamosi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’