Msafara wa wachezaji 19 na viongozi saba wa benchi la ufundi unaondoka usiku wa leo kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabinbwa barani Afrika dhidi ya Zesco
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 28 kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu inaelekea Zambia ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri
Msafara wa kwanza uliojumuisha baadhi ya viongozi wa timu hiyo tayari ulishatangulia nchini Zambia
Aidha, msafara wa mashabiki utaondoka kesho kwenda kuipa nguvu timu katika mchezo huo ambao Yanga inahitaji ushindi au matokeo ya sare ya kuanzia mabao mawili ili waweze kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE