Afisa wa Uhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema ujio wake katika klabu hiyo tayari umewatia hofu wale waliokuwa wamezoea kuinyanyasa Yanga
Akizungumza leo Makao Makuu ya klabu baada ya kutambulishwa rasmi na uongozi wa Yanga, Nugaz amesema amekuja kuirejesha heshima ya Yanga mahali pake
"Lazima waogope kwa sababu wanajua chuma kimetua. Nawaambia kabisa wape salamu, waliinyanyasa sana Yanga hapa kati"
"Waambie mimi nitaongea kiweledi na sio mropokaji. Nitaongea kwa sauti ya Mamlaka kwamba msemaji Kasema"
"Hivyo ndivyo tunavyoanza. Sisi hatushindani, Yanga unyonge na ubariki kwishaa..."
"Uzuri maafisa wote tulioteuliwa ni weledi. Hassani ni mweledi na mimi pia ni mweledi tena mwenye mafanikio na kipato..!"
Hassani Bumbuli amekuwa Afisa Habari wa Yanga akichukua nafasi ya Dismas Ten ambaye bado anashikilia nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu
Nugaz ndiye Afisa wa Uhamasishaji na hakika kazi hiyo ameianza rasmi leo kwenye MKutano na waandishi wa habari