Wakati washambuliaji wapya wa Yanga wakishindwa kuibeba timu yao katika michezo mbalimbali, aliyekuwa kinara wa mabao wa timu hiyo Heritier Makambo nae mambo bado hayajamnyookea nchini Guinea
Makambo alisajiliwa na Horoya Ac mwishoni mwa msimu uliopita akitokea klabu ya Yanga ambayo aliifungia mabao 23 katika mashindano yote
Licha ya kupata nafasi katika michezo kadhaa ikiwemo ya ligi ya mabingwa, Makambo bado hajaifungia timu hiyo
Mshambuliaji huyo pengine nae atahitaji muda kuweza kuzoea mazingira ya Guinea kabla ya kuanza kuonyesha makali yake
Makambo alikuwa kiongozi wa safu ya ushambuliaji ya Yanga, uwezo wake kwenye kufunga uliifanya Horoya Ac itoe kitita cha zaidi ya Milioni 180 kumsajili
Kuondoka kwake Yanga kumetoa nafasi kwa washambuliaji wengine kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria
Sadney Khoutage, Juma Balinya, Maybin Kalengo na David Molinga ni miongoni mwa washambuliaji wapya waliosajiliwa na Yanga