Kagera Sugar imeendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Mbao Fc bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Nyamagana
Bao pekee la Kagera Sugar lilifungwa Awesu Awesu
Kagera Sugar imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama tisa ikishinda michezo yake yote mitatu
Nayo Namungo Fc leo imepunguzwa kasi na Mwadui Fc baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana
JKT Tanzania na Mtibwa Sugar zimegawana pointi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana
Matokeo ya sare pia yamepatikana kwenye michezo ya Mbeya City dhidi ya Ruvu Shooting (1-1) na Ndanda Fc dhidi ya Singida United (1-1)
Yanga haikushuka dimbani wikiendi hii kutokana na wachezaji wake watano kuitwa timu ya Taifa itakayocheza na Sudan hapo kesho
Mabingwa hao wa kihistoria watarejea kwenye ligi mwanzoni mwa mwezi ujao, wakitarajiwa kucheza na Polisi Tanzania Oktoba 03