Kabla ya kuelekea Zambia, wachezaji wa Yanga watakutana na wadau walioandaliwa na kamati ya Hamasa ambao watawajenga wachezaji kisaikolojia
Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na wachezaji waliowahi kutamba na klabu ya Yanga miaka ya nyuma
Pia wachezaji watapata somo kutoka kwa mtaalam wa Saikolojia
Katibu wa Kamati ya Hamasa, Deo Mutta amesema wamedhamiria kuona timu inapata matokeo nchini Zambia
Pamoja na maandalizi ya ndani ya uwanja, ni vyema wachezaji kupewa maandalizi zaidi ya kiakili ambayo yatawafanya waongeze kujiamini
"Tumejifunza mengi katika michuano hii mikubwa ya kimataifa na hasa katika michezo ya hapa nyumbani ambayo imekuwa migumu kwetu kupata matokeo mazuri ya ushindi"
"Hiyo inatokana na mashabiki wetu kutaka matokeo mazuri kwa haraka hali inayosababisha wachezaji wacheze kwa hofu na presha kubwa, hiyo ndiyo sababu kubwa sisi tusifanye vizuri nyumbani na kingine mechi zetu kuchezwa na baadhi wapinzani wetu ni lazima ugumu utakuwepo," amesema
"Tunakwenda Zambia ni matarajio yetu kuona timu inarejea nyumbani kwa ushindi na hilo linawezekana kabisa, tayari tumeanza maandalizi hayo kwa kuanzia na wachezaji ambao wikiendi hii tunatarajia kukutana nao kama viongozi pamoja na mtaalam wa saikolojia"
"Kazi kubwa ya mtaalam huyo ni kuwajengea hali ya kujiamini kwamba inawezekana timu kupata matokeo mazuri ya ushindi, licha ya hapa nyumbani kupata sare ya bao 1-1 na hilo liwezekana kwao kama waliweza kuwafunga nyumbani Township Rollers ya Botswana"