Silaha ya Zesco ni mashambulizi ya kushitukiza - Maguli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2019
Silaha ya Zesco ni mashambulizi ya kushitukiza - Maguli

Mshambuliaji Mtanzania anayekipiga Nakambala Fc inayoshiriki ligi kuu ya Zambia, Elias Maguli amesema uimara wa Zesco United ni kupitia mashambulizi ya kushitukiza wakitumia washambuliaji wao wa pembeni ambao wana kasi

Baada ya kucheza na Yanga, juzi Zesco ilirejea kwenye ligi kuu ya Zambia ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nakambala

Maguli amesema silaha ya Zesco wakiwa nyumbani ni uhodari wao wa kushambulia kupitia pembeni pamoja na mashambulizi ya kushitukiza

"Mabao tuliofungwa sisi yalikuwa ya mashambulizi ya pembeni katika mchezo na Yanga ninachokifikiria ni Zesco watakuwa wanacheza kaunti ataki ili kuwalazimisha Yanga kufanya makosa," Maguli amenukuliwa na Mwanaspoti

"Mawinga wao wana kasi na ndio waliotufunga kwa namna hiyo, lazima Yanga watulie ili kupata ushindi dhidi ya hawa jamaa,lasivyo wanapaswa kujua kwamba sio wepesi"

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Yanga ilifanikiwa kuwabana Zesco kwenye kipindi cha kwanza na pengine wangeweza kufunga mabao mengi kama wangetumia nafasi walizopata

Baadae kwenye kipindi cha pili Zesco walionekana kutawala mchezo zaidi huku Yanga wakishambulia kwa kushitukiza

Uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga ulikuwa sababu ya Yanga kupata matokeo kwenye mchezo huo licha ya Zesco kusawazisha dakika za majeruhi

Mabingwa hao wa kihistoria wanajifua wakapate matokeo kwenye mchezo wa ugenini utakaopigwa Septemba 28

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’